Marekan imeagiza wafanyakazi wasio wa muhimu wa ubalozi wake kuondoka Abuja kutokana na kuongezeka kwa hatari za kiusalama.
Licha ya ahadi ya awali ya United States kusaidia Nigeria kukabiliana na mgogoro wa ugaidi, hali ya usalama nchini humo imeendelea kuwa tete.
Katika hatua ya hivi karibuni, Washington imeagiza wafanyakazi wasio wa muhimu wa ubalozi wake pamoja na familia zao kuondoka Abuja, ikieleza kuwa uamuzi huo unalenga kulinda maisha yao kutokana na kuongezeka kwa hatari.
Hatua hiyo imeibua maswali kuhusu maendeleo ya mapambano dhidi ya ugaidi, hasa baada ya juhudi za kimataifa za kutoa mafunzo na msaada wa kijasusi kwa vikosi vya Nigeria. Wataalamu wanasema kuwa uamuzi huo hauimaanishi kuondoka kabisa kwa Marekani, bali ni hatua ya tahadhari katika mazingira hatarishi.
Chanzo: Newstimehub