Sport
Dollar
38,8028
0 %Euro
43,4936
0 %Gram Gold
4.054,0100
0.01 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Mwanasiasa wa Afghanistan Abdul Zahir Qadir anakabiliwa na mashtaka kuhusu dawa za kulevya na silaha nchini Marekani lakini mawakili wake wanapinga kuwa ushahidi uliowasilishwa dhidi yake umechochewa kisiasa.
Siku ya Jumanne mahakama nchini Kenya iliidhinisha kusafirishwa kwa Abdul Zahir Qadir, aliyewahi kuwa naibu spika wa bunge la Afghanistan, hadi Marekani ambapo anatakiwa kwa mashtaka yanayohusiana na dawa za kulevya na silaha.
Mahakama hiyo katika mji mkuu, Nairobi, imepata ushahidi wa kutosha wa kuidhinisha kusafirishwa kwake baada ya mamlaka nchini Marekani kuwasilisha nyaraka zilizoeleza uhalifu katika mataifa mbalimbali, ikiwemo ulanguzi wa kiwango kikubwa cha dawa za kulevya na usambazaji wa silaha haramu.
Katika hukumu yake, Hakimu BenMark Ekhubi alisema upande wa mashtaka umewasilisha ushahidi wa kutosha wa kusafirishwa kwa Qadir ikiwa ni jukumu la Kenya katika ushirikiano wa sheria ya kimataifa.
Qadir amekanusha madai hayo na anatarajiwa kukata rufaa.
‘Yamechochewa kisiasa’
Wakati wa kesi hiyo, mawakili wake walisema kuwa kusafirishwa kutakiuka haki zake na kuutaja ushahidi huo kama uliochochewa kisiasa.
Hata hivyo, hakimu huyo alitupilia mbali pingamizi hizo na kuamua kuwa Qadir anatakiwa kukabidhiwa, huku hatua zingine za kisheria zikiendelea.
Qadir alikamatwa katika hoteli mmoja mjini Nairobi mwezi Aprili, muda mfupi baada ya kuwasili Kenya, kufuatia ombi la idara ya kupambana na dawa za kulevya ya nchini Marekani (DEA), wakiwa na hati ya kumkamata ya kimataifa iliyotolewa na mahakama mmoja ya jijini New York.
Maafisa wa Kenya wanasema kesi inaonesha jukumu la nchi hiyo ya Afrika Mashariki katika utekelezaji wa haki kwa kutokana na makubaliano ya kimataifa.
Qadir alikuwa katika bunge la Afghanistan hadi 2021, mwaka huohuo ambao Taliban walirejea kuchukua uongozi wa nchi.
Comments
No comments Yet
Comment