Dollar

41,3006

0.16 %

Euro

48,9492

-0.08 %

Gram Gold

4.872,7700

-0.41 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Mahakama kuu nchini Afrika Kusini imetupilia mbali rufaa ya familia ya marehemu Rais wa Zambia Edgar Lungu iliyotaka kusimamisha kurejeshwa kwa mwili wake Zambia kwa mazishi.

Mahakama ya Afrika Kusini yatupa nje kesi ya kukataza mwili wa Lungu kurudishwa Zambia

Mahakama Kuu nchini Afrika Kusini ilitupilia mbali rufaa siku ya Jumanne iliyowasilishwa na familia ya aliyekuwa Rais wa Zambia, Edgar Lungu, iliyokuwa ikitaka kusitisha urejeshaji wa mwili wake nchini Zambia kwa mazishi.

Familia hiyo ilifikisha suala hilo katika mahakama ya Pretoria kupinga uamuzi wa awali ulioruhusu serikali ya Zambia kurejesha mwili wa Lungu nchini humo kwa mazishi ya kitaifa.

Familia ilikuwa na matumaini ya kupeleka suala hilo katika Mahakama ya Rufaa ya Juu (SCA), lakini ombi lao lilikataliwa na mahakama hiyo pamoja na kuamriwa kulipa gharama za kesi.

Mahakama ilisema kuwa hakukuwa na uwezekano wa mafanikio kwa rufaa hiyo.

Maslahi ya Kitaifa

Lungu, mwenye umri wa miaka 68, alifariki Juni 5 wakati akipokea matibabu maalum nchini Afrika Kusini, ambako mwili wake umekuwa ukihifadhiwa.

Familia ilidai kuwa Mahakama Kuu ya Pretoria ilikosea kwa kutumia sheria za Zambia katika mzozo huo kati yao na serikali, badala ya kutegemea sheria za Afrika Kusini.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#