Sport
Dollar
40,4169
0.02 %Euro
47,5317
0.53 %Gram Gold
4.459,4900
1.09 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Hii ni simulizi ya Isaac Imaka, ambaye aliamua kuachana na uandishi wa habari, na kuamua kuingia kwenye siasa akiwa na ndoto za kuwa mbunge.
Mwezi Juni mwaka 2017, aliamua kuacha kazi yake ya uandishi wa habari za bungeni kwenye gazeti la Daily Monitor la nchini Uganda, kazi iliyokuwa inamlipa vizuri kutokana na uzoefu wake wa muda mrefu katika tasnia habari.
Hata hivyo, uamuzi huo uliwashangaza wengi, hata wenzake kudhani kuwa amechanganyikiwa.
“Nilikuwa nimerejea kutoka Marekani ambako nilihudhuria program ya mwaka mmoja iitwayo Alfred Friendly Press Partners Fellowship, nikipata fursa ya kufanya kazi na gazeti la Miami Herald la nchini humo na vile vile kuwa sehemu ya Chuo Kikuu ca Missouri,” anaeleza Isaac Imaka, katika mahojiano yake na TRT Afrika.
Imaka bado anakumbuka namna alivyolazimika kuanzisha taasisi ya maendeleo ya jamii, ili iweze kumsaidia kupata ada, kwani ndio alikuwa ametoka kujiiunga na Chuo Kikuu cha Makerere, mwezi Agosti 2007, kwa ajili ya masomo ya shahada ya Mawasiliano ya Umma.
Katika mahojiano yake na TRT Afrika, Imaka anasema kuwa lengo la taasisi hiyo ilikuwa ni kuwasaidia wazazi kupata fedha za kujikimu, wao pamoja na watoto wao, ikiwemo upatikanaji wa ada za shule.

“Hadi namaliza chuo mwezi Januari 2010, taasisi hiyo iliweza kusaidia zaidi ya watoto 1000 kuendelea na masomo yao ya kidato cha sita,” anaeleza.
Kupitia taasisi hiyo hiyo, Imaka alisaidia ujenzi wa wodi ya akinamama wajawazito, katika eneo la Kaskazini mwa Jinja, nchini Uganda.
Kuwa sehemu ya jamii
Katika miaka saba ya uandishi wa habari nchini Uganda, Imaka anasema kuwa alihisi kwamba alikuwa ameitelekeza jamii yake kwa kiasi fulani.
“Ningekuwa wapi kama nisingeendelea kusaidia wanajamii wezangu kama nilivyofanya wakati nipo chuo kikuu…niliwaza kama ilikuwa vyema kutanguliza maslahi yangu badala ya jamii yangu,” anasema.
Fikra hizo, zikampelekea Imaka kufanya maaumizi magumu, ya kuachana na kazi ya uandishi wa habari, ambayo kama alivyokiri mwenyewe, ilikuwa na maslahi mazuri tu.
Mwanzo wa safari
Mwaka 2018, Imaka alipata fursa ya kukutana na mtawala wa jamii ya Wabusoga wa nchini Uganda, maarufu kama ‘Kyabazinga wa Busoga’, William Nadiope wa IV, na likapatikana wazo la kuanzisha mfuko maalumu wa Gabula, huku Imaka mwenyewe akipewa jukumu la kuusimamia.
Jukumu lake kubwa katika mfuko huo, lilikuwa kuutunisha mfuko huo kwa ajili ya maaendeleo ya watu wa Busoga, hususani wanaopatikana Jinja Kaskazini.
Kupitia taasisi hiyo, Imaka alifanikisha uanzishwaji wa jarida maalumu la jamii ya Wabusoga, linalofahamika kama Busoga Today.
Pia, alifanikiwa kuchochea uanzishwaji wa michezo ya sarakasi kwa wazee, majadiliano ya amani maarufu kama ‘Ebikomi’ na utumiaji wa michezo kama nyenzo ya kupunguza, kama sio kuondoa kabisa mimba za utotoni.

Uamuzi wa kuwania ubunge
Kulingana na Imaka, uamuzi wa kugombea ubunge wa Jinja Kaskazini ulichochewa na uelewa wake mkubwa katika shughuli na vikao mbalimbali vya bunge la nchi ya Uganda, hasa ukizingatia kuwa alikuwa ni mhariri wa habari, wakati akiifanyia kazi kampuni ya Daily Monitor ya nchi hiyo.
“Nikiwa ndani ya ukumbi wa bunge, niliweza kuona umuhimu wa mhimili huo na namna linavyotumika kutunga sheria…niliwaza moyoni kuwa ningeweza kutumia fursa hiyo kuibaildi kabisa jamii yangu,”anaiambia TRT Afrika.
Anasisitiza kuwa jamii ya Busoga inakabiliwa na changamoto kubwa ya uongozi, na hivyo kuwafanya watu wa eneo hilo wakose maendeleo.
Anasema: Mwanasiasa ambaye hana uwezo wa kufanya msaragambo kwa jamii yake atabaki kuongelea tu vipaumbele vyake bila kuvitekeleza.
Imaka anaongeza kuwa mbunge mwenye ufanisi katika uongozi ni yule mwenye kuelewa matatizo ya watu wake, kwa lengo la kuyatafutia utatuzi.

Vipaumbele vyake
Anapojiandaa na uchaguzi mkuu wa Uganda, uliopangwa kufanyika Januari 12 hadi Februari 9, 2026, kati ya mambo mengine, Imaka amenuia kupambana na umasikini, ukosefu wa ajira na magonjwa katika jamii yake, jambo ambalo anaamini kuwa atalitekeleza kupitia ukuzwaji wa elimu ya biashara kilimo kwa watu wa eneo hilo.
Pia analenga kukuza vipaji kupitia sanaa na michezo, akiamini kuwa ni njia bora ya kujitengeneza fursa za kujiajiri kwa watu wa Jinja Kaskazini, hususani jamii ya Busoga.

“Tunatamani sana kuona kuona vijana wetu wakitumia vipaji vyao kutamba katika majukwaa ya kimataifa,” anaeleza.
Hali kadhalika, amelenga kutumia timu maalumu za afya katika kupambana na magonjwa katika eneo la Jinja Kaskazini.
Comments
No comments Yet
Comment