Samukele Kabini alifunga zikiwa zimesalia dakika 13 na kuipa Afrika Kusini ushindi wa 2-1 dhidi ya Guinea, huku Eritrea ikitoka sare ya 1-1 na Kenya mjini Nairobi.
Afrika Kusini ilianza mechi za Kundi D kwa ushindi wa 2-1 nyumbani dhidi ya Guinea mjini Soweto, baada ya Samukele Kabini kufunga bao lake la kwanza la kimataifa zikiwa zimesalia dakika 13.
Beki Ime Okon aliipa Afrika Kusini uongozi kabla ya Seydouba Cisse kuisawazishia Guinea. Baadaye, Yanela Mbuthuma aliyeingia akitokea benchi alimpenyezea Kabini nyuma ya safu ya ulinzi na Kabini akamalizia mpira wavuni.
Mjini Nairobi, Eritrea na Kenya zilitoka sare ya 1-1. Nahom Girmai aliipa Eritrea uongozi kabla ya Ryan Ogam kusawazisha zikiwa zimesalia dakika tatu.
Michezo
