Jeshi lasema lina uwezo wa kulinda Hormuz dhidi ya vitisho vya Marekani na Israel.

Iran yakataa  uingiliaji wa nje katika usalama wa Ghuba ya uajemi

Mamlaka za kijeshi za Iran zimetangaza kuwa hakuna haja ya mataifa ya kigeni kuingilia usalama wa Ghuba ya Uajemi, zikieleza kuwa wao pamoja na washirika wao wanaweza kukabiliana na vitisho vyovyote.

Iran imesisitiza kuwa udhibiti wake katika Mlango wa Hormuz uko imara, huku ikionya dhidi ya jaribio lolote la kuingilia masuala ya eneo hilo.
Kauli hiyo imekuja wakati mvutano kati ya Iran na mataifa ya Magharibi ukiendelea kuongezeka, hasa kufuatia mashambulizi ya hivi karibuni.

CHANZO: Newstimehub

#