FIFA imesema Iran itashiriki mashindano ya Kombe la Dunia licha ya changamoto za kisiasa
FIFA imethibitisha kuwa Iran itakuwa sehemu ya FIFA World Cup 2026, hatua iliyotangazwa na rais wake Gianni Infantino.
Infantino alieleza kuwa Iran "itashiriki kwa hakika", akisisitiza kuwa michezo inapaswa kuunganisha dunia badala ya kugawanya kutokana na siasa,Mashindano hayo yatakayofanyika kwa pamoja katika United States, Canada na Mexico yanatarajiwa kuwa ya kipekee kutokana na kushirikisha timu 48 kwa mara ya kwanza.
Licha ya mvutano wa kisiasa na changamoto za usafıri kwa baadhi ya maafısa, FIFA imeweka wazi kuwa timu ya taifa ya Iran haitazuiwa kushiriki katika mashindano hayo makubwa.Hatua hiyo imepokelewa kwa mitazamo tofauti, lakini inaonyesha msimamo wa FIFA wa kutenganisha michezo na siasa.
Chanzo:Newstimeshub