Maandamano dhidi ya wahamiaji wasiokuwa na vibali yameongezeka huku wananchi wakilalamikia hali ngumu ya maisha.
Hali ya taharuki imeongezeka nchini South Africa baada ya makundi ya wananchi kuandamana kupinga kile wanachokiita ongezeko la uhamiaji haramu,waandamanaji walieleza kuwa wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa ajira na wanahisi kuwa wahamiaji wanachangia ushindani mkubwa katika soko la ajira pamoja na biashara ndogo ndogo. Wengine walidai kuwa huduma za kijamii kama afya na makazi zimeelemewa kutokana na ongezeko la watu,
Katika baadhi ya maeneo, kulikuwa na hofu ya kutokea kwa vurugu kutokana na historia ya matukio ya chuki dhidi ya wageni, ambapo maduka ya wahamiaji yamewahi kushambuliwa au kufungwa kwa nguvu,serikali imewataka wananchi kudumisha amani na kuacha kuchukua sheria mkononi, ikiahidi kushughulikia suala la uhamiaji kwa njia za kisheria na za utaratibu. Polisi pia wameongeza doria ili kuzuia hali yoyote ya vurugu.
Mashirika ya kiraia yameonya kuwa hatua za kihisia zinaweza kuongeza mgawanyiko katika jamii na kusababisha madhara makubwa kwa watu wasio na hatia.
Chanzo:Newstimeshub