Wahamiaji wengi wanahatarisha maisha yao kwa kukabiliwa na njaa na ajali za baharini wakielekea Yemen.

Hatari Yaongezeka Kwa Wahamiaji Kwenye Njia ya Yemen.

Watu wengi kutoka eneo Pembe ya Afrika wanaendelea kuhatarisha maisha yao wakisafıri kuelekea Yemen kupitia bahari, wakikabiliwa na njaa na ajali mbaya.

Kwa mujibu wa mashirika ya kimataifa, safari hiyo imekuwa moja ya njia hatari zaidi za uhamiaji duniani, huku wahamiaji wakikosa mahitaji ya msingi kama chakula, maji na huduma za afya.

Baadhi ya wahamiaji hulazimika kusafiri kwa siku kadhaa katika mazingira magumu, hali inayosababisha vifo vya wengi kutokana na uchovu na njaa,Aidha, boti wanazotumia mara nyingi huwa dhaifu na zisizo salama, jambo linaloongeza hatari ya kuzama baharini.

Mashirika ya kibinadamu yanatoa wito kwa serikali na jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za kulinda maisha ya wahamiaji na kushughulikia sababu zinazowalazimisha kuhama.

Chanzo:Newstimeshub 

#