Soko la nishati latikiswa huku wawekezaji wakihofia mkwamo wa muda mrefu Mashariki ya Kati.
Wasiwasi kuhusu hatma ya Mlango Bahari wa Hormuz umeendelea kusukuma juu bei ya mafuta nchini Marekani baada ya mkutano wa dharura wa Rais Donald Trump na viongozi wa sekta ya nishati.
Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni, wastani wa bei ya petroli nchini Marekani umefikia takribani dola 4.23 kwa galoni, kiwango cha juu zaidi katika miaka kadhaa.
Wachambuzi wanasema hofu ya kusambaratika kwa usafirishaji wa mafuta kupitia Hormuz imeongeza presha katika masoko ya kimataifa ya nishati.
Iwapo mkwamo huo utaendelea, wataalamu wanaonya kuwa gharama za mafuta zinaweza kuendelea kupanda katika wiki zijazo.
CHANZO: Newstimehub