Dollar

40,2237

0.07 %

Euro

47,1146

0.08 %

Gram Gold

4.338,1200

0.07 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Balozi Humphrey Hesron Polepole pia alilalamikia kutovuka kwa maadili na sera za chama tawala CCM akiashiria hususan mchakato wa uteuzi wa wagombea ndani ya Chama uliomalizika hivi karibuni.

Balozi wa Tanzania nchini Cuba ajiuzulu akilalamikia kufifia maadili katika serikali ya awamu ya 5

Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Hesron Polepole, ametangaza rasmi kujiuzulu nafasi yake ya kidiplomasia na uongozi wa umma, akitaja kukosekana kwa uelekeo sahihi katika uongozi wa kitaifa, kufifia kwa maadili katika ngazi mbali mbali serikalini na kutoheshimiwa haki za raia.

Balozi Polepole ameelezea malalamiko yake katika barua ndefu aliyotuma rasmi kwa mwajiri wake Rais Samia Suluhu Hassan huku akielezea mambo mengi yaliyomkirihisha kuendelea kuhudumu ndani ya serikali.

‘‘Kwa muda wote wa kuhudumu ndani na nje ya nchi, nimefuatilia kwa karibu na kushuhudia kwa masikitiko makubwa mwelekeo wa uongozi usiojielekeza ipasavyo katika kusimamia Haki za watu, Amani na kuheshimu watu, kufifia kwa dhamira ya kweli na uwajibikaji wa dhati wa kushughulikia kero na changamoto zao, na kudidimia kwa maadili ya uongozi katika ngazi mbalimbali,’’ alielezea Balozi Polepole.

Humphrey Hesron Polepole amehudumu katika wadhifa huo akisimamia maeneo ya Cuba, pamoja na uwakilishi wa eneo la Karibe, Amerika ya Kati na nchi rafiki za Colombia, Venezuela na Guyana, tangu alipoteuliwa Aprili 2023.

Chama kwanzam mtu baadaye - CCM

Balozi Polepole amelalamika kuwa mwenendo wa utawala uliopo sasa umemkosesha amani na imani na uongozi aliopo ndani yake.

Pia alilalamikia kutovuka kwa maadili na sera za chama tawala CCM akiashiria hususan mchakato wa uteuzi wa wagombea ndani ya Chama uliomalizika hivi karibuni.

‘‘Imekuwepo kauli maarufu ya CCM isemayo “Chama kwanza mtu baadaye”, mwanzoni mwa mwaka huu, nilipoona kauli hii inafanyika vinginevyo, nimejiuliza mara kadhaa ni maslahi ya nani yanapiganiwa wakati huu, mtu, kikundi au Chama Taasisi?’’ ameuliza Polepole.

Kabla ya uteuzi wake Cuba, Balozi Polepole alihudumu kama Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Novemba 2020 – Machi 2022), na hatimaye kama Balozi katika vituo vya Lilongwe – Malawi (Machi 2022 – Aprili 2023).

Alihitimisha kwa kusema kuwa ataendelea kuwa mwanachama wa CCM.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#