Boti imepinduka katika mto Nguse Uganda, huku watu wengi wakihofiwa kufariki na wengine kupotea.

Ajali ya Boti Uganda Yaua Watu Kadhaa, Wengine Wapotea

Ajali mbaya ya majini imetokea katika Nguse River nchini Uganda baada ya boti kupinduka na kusababisha vifo vya watu kadhaa huku wengine wakipotea.

Taarifa zinaeleza kuwa boti hiyo ilikuwa imejaa kupita kiasi na huenda pia hali ya hewa au mikondo ya maji ilichangia ajali hiyo. Watu waliokuwemo ndani ya boti walikuwa wakivuka kutoka upande mmoja wa mto kwenda mwingine wakati tukio hilo lilipotokea.

Mashuhuda wanasema kuwa baadhi ya abiria walijaribu kuogelea kujiokoa, lakini wengi wao hawakuwa na uwezo wa kufanya hivyo kutokana na nguvu ya maji.

Vikosi vya uokoaji vinaendelea na juhudi za kuwatafuta waliopotea huku vikisaidiwa na wananchi wa eneo hilo. Serikali imeeleza masikitiko yake na kuahidi kuchukua hatua kali dhidi ya ukiukwaji wa sheria za usafıri wa majini ,wataalamu wanasema kuwa ajali nyingi za aina hii hutokana na uzembe wa waendeshaji pamoja na ukosefu wa vifaa vya usalama.

Chanzo:Newstimeshub 

#