Viongozi wa dunia, hasa kutoka barani Afrika na Mataifa yanayoendelea, wamehoji kuwa shirika lililoundwa miaka 80 iliopita haliendani na dunia ilivyo kwa sasa.

Afrika itapatana hadhi ya uwanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa?

Wito wa kufanyika kwa mabadiliko katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa unasikika tena katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa. 

Lakini hili siyo suala geni. Kwa miongo kadhaa, viongozi wa dunia, hasa kutoka Afrika na mataifa yanayoendelea, wamedai kuwa shirika lililoundwa zaidi ya miaka 80 iliopita haliendani na dunia ilivyo kwa sasa. 

Ujumbe huu umerudiwa na viongozi wa zamani na wa sasa."Tumeomba na kuomba: mabadiliko, mabadiliko katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa," aliyekuwa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe alisema katika moja ya hotuba zake kwa Mkutano wa Umoja wa Mataifa. 

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amekuwa akiuweka ujumbe wake huo kwa kauli moja: "Dunia ni kubwa kuliko nchi tano." 

Na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeondoka António Guterres pia ametoa wito kwa Baraza hilo "kwenda na wakati."

Kura ya turufu iwe kwa mataifa kadhaa

Pia kuna kutoelewana kuhusu nani apewe hadhi ya mwanachama wa kudumu na kama watakuwa na uwezo wa kura ya turufu. 

Mataifa matano ya sasa hayataki uwezo wa kura ya turufu upewe nchi zingine, huku wengine ambao siyo wanachama wa kudumu wakitaka hadhi hiyo iondolewe kabisa.

Hata hivyo, Afrika inaendelea kushinikiza hilo, ikitaka kupewa angalau nafasi mbili za uanachama wa kudumu. India, Brazil, Ujerumani na Japan pia zimetaka kujumuishwa kwenye nafasi hiyo, huku wengine wakitaka iwepo tu kwa mataifa ya kupigiwa kura.

Baraza hilo liliongeza idadi ya wanachama kutoka 11 hadi 15 mwaka 1965, lakini kwa uanachama wa kudumu haujabadilika tangu 1945.

Kufikia sasa baada ya miongo kadhaa ya kutolewa kwa wito huo, badi kuna utata: kunakuwa vipi na mgawanyiko wa uwezo wakati wale walio katika nafasi wanaamua kama kuna umuhimu wa kufanya hivyo?

#